Mbunge wa Iringa mjini kwa tiket ya CHADEMA Mchungaji Petter Msigwa amehoji kwanini bendera za vyama vya upinzani
zinang’olewa kwa nguvu na kuwekwa za CCM kwenye maeneo yote ambayo Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapopita kwenye ziara yake kikazi.
Msigwa aliuliza swali wakati wa kipindi cha
maswali na majibu mapema leo Aprili 12, 2019 bungeni jijini Dodoma.
Kwa upande mwingine, Mbunge wa Kibamba kwa
tiketi ya CHADEMA, Mhe. John Mnyika amehoji ni kwanini Wabunge hawajagawiwa
ripoti mpya ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) kama kanuni za Bunge zinavyosema.
Mnyika ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma
leo Aprili 12, alipokuwa akiomba mwongozo wa Spika Utawala Bora, ambapo amesema
kwamba kitendo cha wabunge kutogawiwa ripoti hiyo hakiwezi kuungwa mkono na
wabunge kwa kuwa kinakiuka kanuni za Bunge.
Hata hivyo, ombi hilo
la Mnyika limegonga mwamba baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kusema
ripoti hizo za CAG haziwezi kugawiwa kwa wabunge kama Mnyika anavyotaka kwa
kuwa kanuni haziruhusu kufanya hivyo.
0 Maoni